Kuitwa Kwenye USAILI

Kampuni ya Reli Tanzania

This is a Full-time position in Dar Es Salaam posted 26/02/2018.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania anatarajia kuendesha usaili kwa waombaji
walioorodheshwa katika tangazo hili na hatimaye kuwapangia kazi waombaji watakaofaulu usaili.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanyika saa1:00 asubuhi kabla ya muda wa mtihani wa mchujo
kuanza.
2. Mtihani wa mchujo utafanyika tarehe 3.3.2018 kuanzia saa moja asubuhi katika ukumbi
wa NIT MABIBO JIJINI DAR ES SALAAM.
3. Unakumbushwa kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha
mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
4. Pia unakumbushwa kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne,
sita, Stashahada, Astashahada, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
8. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
9. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
10. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE)
11. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao
hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Download Names Through


TANGAZO LA KUITWA KATIKA USAILI

How to Apply